Ripoti ya Shirika la AhlulBayt(a.s)ABNA:Ahmed Bani msemaji wa kijeshi wa NTC amesema kuwa Saiful Islam Gaddafi mwana wa kiume wa Muammar Gaddafi dikteta wa zamani wa Libya anapaswa kuhumiwa ndani ya nchi hiyo na kwamba viongozi wa Libya wanapinga kuhukumiwa Saiful Islam katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ICC. Bani ameongeza kuwa viongozi wa Libya wataithibitishia dunia kuwa Walibya ni watu waliostaarabika wanaofuata mifumo ya sheria ya kiadilifu.Hivi karibuni kulichapishwa ripoti mbalimbali kuhusu uamuzi uliochukuliwa na Saiful Islam wa kutaka kujisalimisha katika mahakama ya ICC. Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ya mjini Hague Uholanzi mwezi Juni mwaka huu, ilimtuhumu Saiful Islam Gaddafi kwa kutenda jinai dhidi ya wananchi wa Libya waliokuwa wakiandamana katika mapinduzi ya nchi hiyo. Maafisa wa serikali ya Tripoli wanahofu kuwa Saiful Islam hana nia ya kujisalimisha kwa mahakama ya ICC na kwamba anachokifanya ni kupoteza muda katika jitihada zake za kujaribu kukimbilia katika nchi jirani ya Kiafrika.
19 Machi 2011 - 20:30
Msimbo wa Habari: 275491
Viongozi wa Baraza la Taifa la Mpito la Libya (NTC) wametaka Saiful Islam Gaddafi mwana wa kiume wa dikteta wa zamani wa nchi hiyo ahukumiwe ndani ya Libya.